Mikopo mingi imeenda kwa wasio walengwa na wengi Wanasiasa, niko serikalini najua, wengine wanadaiwa Mabilioni na ndio wapiga kelele’
wakati wa kupiga dili haupo tena, wale wa serikalini waliokua wanapiga dili hawatapiga tena sanasana watapigwa wao. Tuliposimamisha ajira kwa miezi miwili haikua na maana zimezuiliwa, sasa hivi zinaendelea na juzi tumetoa za Madaktari karibu 100’Sasa hivi tunaajiri lakini kwa uangalifu tusije kuwarudisha Watumishi hewa, hizi fedha zilizokua zinawalipa ni fedha za maskini
’
Takwimu za kutosafiri mimi na wengine kiasi gani tumeokoa ijulikane tu ni Mabilioni na isieleweke hatusafiri kabisa, pia tuna MabaloziMsafara wa Rais kwenda nje ya nchi unabeba mpaka watu 40 lakini unapomtuma Waziri unaweza kukuta ni watu wawili
’
Sheria mpya ya huduma za habari, sifahamu Wabunge watachoamua ila sitaki unafiki siku itakayoletwa kwangu siku hiyohiyo nitaisaini’palepale .Vita hivi ni za maslahi, ni bora nisiwe Rais maarufu lakini siku moja mtanikumbuka au nitakua maarufu mbinguni’ Kuhusu katiba mpya niache kwanza niinyooshe nchi, hata kwenye kampeni zangu nilikozunguka hakuna mahali nilizungumzia katiba mpya’ Wanasiasa wanamamidomo kweli utadhani ni wasafi, hizi ni changamoto ambazo naziona
Kuhusu Znz ni shwari wameitisha uchaguzi wao umefanyika vizuri na nchi inaenda ,kila kitu kiko safi na Dr.Shein ndio Rais halali.
Sitokuwepo hapa IKULU milele natengeneza hii nchi kwa ajili ya watanzania tukisimama kwapamoja inchi yetu itafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana
waandishi nyinyi nawapenda sana ndo maana kuna wengine humu nawachagua niko pamoja na nyinyi mjisikie mko nyumbani
Hayo nibaadhi ya mambo amba yo ameyatolea ufafanuli leo IKULU ya Dar es salaam akiwa anahojiwa na waandishi wa habari nawahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
No comments:
Post a Comment