Swali(Tido Mhando): Ulichukua muda kuunda baraza la mawaziri, Je Katika
tathmini hiyo wanafanya kazi kulingana na ulichotegemea wakifanye
Jibu(Magufuli): Serikali niliyonda imenisaidia sana na wanafanya kazi
zao vizuri, niliona niwe na baraza la watu wachache katika kuwatumikia
wananchi, changamoto zipo lakini nina imani kubwa.
Swali(Lulu Sanga
TV 1):Kuna changamoto kubwa sana ya dawa, watoto wengi wanakufa kutokana
na kukosa dawa, unaoneje ukibana matumizi kupata dawa ukazigawa
hospitali kubwa au kampeni kama ile ya madawati.
Jibu(Rais
Magufuli): Katika bajeti yetu tumetenga bilioni 1.99 na tumeongeza
bajeti ya kununulia madawa karibu mara kumi. Tumebadilisha utaratibu
badala ya kununua kutoka kwa suppliers sasa tunanunua moja kwa moja
kutoka viwandani pia kuna nchi zinataka kuwekeza kujenga viwanda vya
kutengeneza madawa hapahapa.
Swali
Jibu: Katika kazi yoyote
Sijakandamiza demokrasia ndio maana unaona bunge linaendelea na chaguzi
zinaendelea hata hapa wamechagua UKAWA, demokrasia ina mipaka yake,
baada ya uchaguzi lazima watu waendelee na production
Swali(Tido)-Nyongeza:Kuna watu wanasema unataka kuelekea kwenye udikteta
JIBU:Tafsiri kila mmoja ana yake na kila mmoja ana uhuru wa kufukiria
anavyofikiria hata wewe Tido ulihama BBC, TBC na sasa uko Azam, mwingine
anaweza kufikiri uko ulikokuwa kulikuwa na udikteta wa aina fulani.
Swali(Rioba):Unasisitiza uchumi wa viwanda, Tanzania imeshawahi kuwa na
viwanda vikafa, kuna watu wanaona hili swala waachiwe watu binafsi,
wewe unaoneje?
Jibu
Ilani inasema tunataka kujenga nchi ya
viwanda, huwezi kutegemea serikali katika kujenga viwanda ndio maana
nikasema kuna makampuni kutoka Kenya na sio makampuni ya watu binafsi.
Swali(Mtanzania)Serikali imeweka mkazo kwenye kupambana na majangili lakini tishio ni kubwa,
Jibu(Rais Magufuli): Umezungumza ukweli na ni changamoto ila pia ina
historia yake, sheria ya mifugo ya mwaka 59 ila tumejipanga kuhakikisha
haya masuala yasije yakawa parmanent na tumeibadilisha wizara ya
maliasili na nimeteua majenerali kuongoza wizara nadhani umeshajua
tunataka kufanya nini. Hatuna viwanda vya nyama nchi hii ndio maana
mifugo haina pakwenda.
Swali(Magazeti ya serikali):Ni nini mkakati wa kuwafanya watanzania kuona fursa katika sekta nyingine
Jibu(Rais Magufuli):Sisi kama serikali ni kuwaelimisha waweze kutumia
fursa zilizopo katika nchi nyingine, mfano sisi tunasifika kwenye
Kiswahili, kila mmoja ajipange badala ya kusubiri serikali. Fursa zipo
ikiwemo EAC na SADC ambako Tanzania ni mwanachama. Ni wajibu sisi wa
wwatanzani
Swali(Tido Mhando): Ulitilia mkazo Rushwa na ufisadi, mwaka mmoja sasa unasemaje?
Jibu(Rais Magufuli):Matunda yameanza kuonekana, nidhamu kazini imeanza
kuonekana, tumepitisha sheria ya mafisadi na kesi ya kwanza imeanza
kusikilizwa jana. Rushwa na swala mtambuka na haliwezi kushughulikiwa na
Rais peke yake. Nitoe wito kwa watanzania wote tukatae Rushwa, ni kansa
ya maendeleo.
Swali(Rioba)Kuna maswala umeyasimamia kwa ujasiri ikiwemo ujangili na dawa za kulevya, nini kinakuumiza kichwa
Jibu(Rais Magufuli)Yanayoniumizwa kichwa ni mengi pamoja na swali lako,
yale niyoahidi katika miaka mitano bado sijayamaliza na hayawezi
kumalizika ndani ya mwaka mmoja. Kwenda mbele unahitaji support ya watu
wengi. Mwenyezi Mungu pamoja na support ya watanzania.
Swali(Tuma-Radio Tumaini
Hongera sana, Kura yangu ilifanya kazi, Walemavu wa chini hali bado ni
mbaya, tunazo sheria nyingi tunaishukuru serikali. Mazingira
yetu(walemavu) bado ni magumu, tunaomba watu wa chini watu iwaangalie.
Jibu(Rais Magufuli): Nimelipokea ombi lako na tutaendelea
kulishughulikia na serikali inajali sana walemavu kwani hata sisi ni
walemavu wa kesho, nimeunda wizara maalum ya walemuavu, nimewateua
walemavu katika baraza langu ikiwemo Dr Possy, Amon Mpanju.
Swali(Bakari Machumu Mwananchi): Viwanda na utajiri wa madini, umeelezea
umuhimu wa PPP, kuna wafanyabiashara wanahisi wanatengwa, upande wa
madini, tunaunganisha vipi
Jibu(Rais Magufuli): Wafanyabiashara
hawajatengwa na tunawahitaji sana, na mimi nawapenda kweli
wafanyabiashara lakini nataka wanaolipa kodi. Mfanyabiashara ambae
hajalipa kodi anawaumiza ambao wamelipa kodi, ukishakua na wafabiashara
wa aina mbili unawaumiza wanaolipa. Palikuwa na mamabo ya hovyo, sitaki
kwenda kwenye detail sana maana mambo mengine yapo mahakamani,
wafabiashara matapeli siwapendi.
Jibu(Rais Magufuli): Kuhusu madini,
ni kweli nchi hii ina madini mengi sana, madini yanatakiwa kunufaisha
nchi hii, siku moja yatakwisha, nina uhakika sasa mambo yataanza kwenda
vizuri baada ya kusaini regulations. Sisi tuna mafuta pia, tutaunganisha
bomba la hoima kwenda Tanga, Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini
nchi iliyoongoza kuuza ni India ikifuatiwa na Kenya. Sasa hivi
umeanzishwa mnada hapa. Watu wanasafirisha makontena kwenda nje
kusafishwa na sisi wenyewe tunayasindikiza. Kwa nini tusitengeneze hapa,
haya ndio ndio najaribu kuyazungumza ili nchi yetu isiendelee kuibiwa,
kwenini kila sehemu kwenye madini kuna kiwanja cha ndege, hili sio suala
la Rais pekee ili pesa zinazopatikana ziwanufaishe watanzania wote.
Unachosema ni sawa na kinachotakiwa sasa kusonga mbele.
Swali(Joseph Kulambwa): Tanzania ya viwanda, serikali imejipangaje kutrain mafundi mchundo kuliko wasimamizi wa viawanda
Jibu(Rais Magufuli)Vyuo vya kati tulivibadilisha kuwa vyuo vikuu,
ilikua bad direction ndio maana sasa tunajenga vyuo vya VETA ikiwezekata
kila mkoa. Hata chuo cha usafirishaji kimekua chuo kikuu na inawezakana
kwa sababu kulikua na mikopo ambayo hairudishwi ndio maana sasa kuna
deni la trilioni 3.5.
Swali: Wafanyakazi hewa wameondolewa lakini bado mishahara inayolipwa ni mikubwa?
Jibu(Rais Magufuli)Siku za nyuma kuna madai mengi ambayo yamepelekea
serikali kulipa kiasi cha bilion 22.6 na bado kuna madai 39,000 yenye
thamani ya sh bilioni 23
Suala la OC bado halitakuwepo kwani mambo yanaenda vizuri.
Aidha serikali itaendele kulipa madeni ya walimu na wakandarasi wanaodai.
Swali(Angalieni Mpendu): Suala la utamaduni na maadili, umeliwekaji katika utawala wako?
Jibu(Rais Magufuli) Jukumu la ku-maintain utamaduni wetu ni la kila
mtanzania, kuna wizara inayoshughulika suala hili. Kila mtanzania ana
wajibu wa kutunza utamaduni wetu.
Vyombo vya habari vitoe ushrikiano kwa kuhakikisha utamaduni wetu unakuwa mzuri.
Swali(Bukuku): Serikali ya china na Tanzania ni Marafiki, Unaonaje kam
ungefanya mazungumzo ma Wachina kukawa na ushirikiano katika mafunzo na
mashine ndogondogo
Jibu(Rais Magufuli): Nimeshazungumza nao, wachina
wamekubali na wanataka kuchukua eneo la Bagamoyo wajenge viwanda 1000.
Pia tumezungumza na serikali ya India katika suala kama hilo hilo.
Tumezungumza na serikali ya Morocco na kutakuwa na ndege ya moja kwa
moja kutoka Kasablanca hadi JNIA.
Post Top Ad
Responsive Ads Here

HABARI >>>>> MAJIBU NA MASWALI YA RAIS IKULU
Share This
Tags
# HABARI
Share This
About gambatheboss
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BREAKINK NEWS>>>>.GAMBATHEBOSS IMERUDI HEWANI
" Tuna ombaradhi wapenzi wa somaji wetu kwa kupotea hewani takribani mwaka mmoja na nusu hivi kutokana na tatizo lililo kuwa nje ...
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment