HABARI>>>>MWILI WA SITTA KUPOKELEWA BUNGENI - G EMPIRE

G  EMPIRE

PATA HABARI ,MATUKIOMBALIMBALI KWA WAKATI MUAFAKA KUPITIA HAPA GAMBATHEBOSS

Latest in Tech

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

HABARI>>>>MWILI WA SITTA KUPOKELEWA BUNGENI

Share This

Jana, Bunge lililazimika kutengua kanuni kuwezesha kumpa heshima za kipekee Sitta aliyekuwa Spika wa Bunge la 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 ambaye leo mwili wake utaingizwa ndani ya Ukumbi wa Bunge kuagwa kwa heshima na wabunge ambao baadhi yao alikuwa nao katika Bunge hilo la Tanzania.

Sitta aliyewahi kuwa pia Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, alifariki usiku wa kuamkia Jumatatu katika Hospitali ya Technical University ya mjini Munich, Ujerumani ambako alikuwa amelazwa akitibiwa saratani ya tezi dume. Alizaliwa Desemba 18, 1942 mjini Urambo.
Mwili wa Sitta uliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) jana saa tisa alasiri ukitokea nchini Ujerumani ambako alienda kwa matibabu. Ulipokewa na baadhi ya viongozi wa serikali, viongozi wastaafu, viongozi wa vyama vya siasa pamoja wananchi waliofika uwanjani hapo.
Kwa hatua hiyo ya kutengua kanuni, Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 utakuwa umetengua kanuni zake kwa mara ya pili; awali kanuni zilitenguliwa juzi Jumanne ili kusitisha shughuli za Bunge baada ya kifo cha Sitta kutangazwa.
Spika wa Bunge, Job Ndugai jana kwa mujibu wa utaratibu na kanuni za Bunge, alimuomba Waziri, Ofisi ya Rais, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama kutengua kanuni ili kuruhusu shughuli za kumuaga Sitta zifanyike ndani ya Ukumbi wa Bunge kwa heshima ya kiongozi huyo.
Kanuni zilizotenguliwa ni ya 139 (1) inayohusu wageni wanaoingia Ukumbi wa Bunge kwamba wataketi maeneo maalumu ya wageni na si katika ukumbi wenyewe na kanuni ya 143 (e)-(f) kuhusu mpangilio wa Bunge wa kukaa, uliowekwa kwa namna ya baadhi ya watu.
Ndugai alimwelezea Sitta ambaye akiongoza Bunge alijipambanua kwa falsafa yake ya Kasi na Viwango, aliyeanzisha matangazo ya mubashara (live) katika Bunge la 10 na kuwaeleza wabunge kuwa, leo shughuli ya kumuaga itakuwa mubashara.
Akielezea utaratibu wa leo, Ndugai alisema wataupokea mwili wa Sitta saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
“Kutakuwa na kikao maalumu cha Bunge saa 8:30 mchana tuwe tumekaa kwa kikao hicho maalumu cha Bung.
Akielezea zaidi alisema baada ya hapo wabunge watatoka nje ya lango kuu, watakakokaa kwa muda mfupi.
“Tutabeba jeneza kwa kushirikiana. Tumepewa saa mbili tu. Tutafanya kumpa heshima kubwa Mzee Sitta. Viongozi wetu wa kitaifa watapewa heshima zote hizo kwa kuletwa bungeni ambako ndiko nyumba ya Watanzania wote ilipo,” alisema Ndugai.

No comments:

Post a Comment

BREAKINK NEWS>>>>.GAMBATHEBOSS IMERUDI HEWANI

     " Tuna ombaradhi wapenzi wa somaji wetu kwa kupotea hewani takribani mwaka mmoja na nusu hivi  kutokana na tatizo lililo kuwa nje ...

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages