Baada ya raisi wa jamhuri ya kidemokrasi ya congo kutua nchini azungumzia haya....
RAIS Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemorasi ya Congo amesema nchi yake itaimarisha biashara na Tanzania ili kukuza uchumi wa nchi hizo.
Rais Kabila amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) jijini Dar es Salaam.
Awali Rais John Magufuli amesema yeyote atakayesababisha wafanyabiasra wa DRC kushindwa kufanya biashara kupitia bandari ya Dar es Salaam atachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo na kumuagiza balozi wa DRC hapa nchini, Jean-Pierre Mutamba kutoa taarifa kwake kuhusu usumbufu wowote watakaopata wafanyabiashara wa nchi hiyo.
Kwa habari zaidi...........
No comments:
Post a Comment