Leo October
28 2016 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Benno Ndullu aliita waandishi
wa habari kwa Dharura, mbele ya waandishi wa Habari ametoa
taarifa kuwa Benki kuu ya Tanzania imechukua usimamizi wa benki ya ‘Twiga Bancorp’ kuanzia October 28 2016
.
Gavana wa
benki hiyo ameeleza kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini kuwa
benki ya Twiga ina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria
ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.
Kutokana
na uamuzi huo benki kuu ya Tanzania imesimamisha bodi ya wakurugenzi na
uongozi wa benki ya Twiga na imemteua Meneja msimamizi ambaye atakuwa na
jukumu la kusimamia shughuli za benki ya Twiga kwa kipindi ambacho
itakuwa chini ya usimamizi wa benki kuu.


No comments:
Post a Comment