MPYA >>>Rais Dr. Magufuli kufanya ziara nchini kenya - G EMPIRE

G  EMPIRE

PATA HABARI ,MATUKIOMBALIMBALI KWA WAKATI MUAFAKA KUPITIA HAPA GAMBATHEBOSS

Latest in Tech

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MPYA >>>Rais Dr. Magufuli kufanya ziara nchini kenya

Share This

Leo Oct 31 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa  Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Rais Dr.Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watafanya mazungumzo.

Pamoja na kufanya mazungumzo  na mwenyeji wake, Rais Magufuli atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Nairobi

Katika ziara hii Rais Dr. Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara  ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

Rais Dr. Magufuli anatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

BREAKINK NEWS>>>>.GAMBATHEBOSS IMERUDI HEWANI

     " Tuna ombaradhi wapenzi wa somaji wetu kwa kupotea hewani takribani mwaka mmoja na nusu hivi  kutokana na tatizo lililo kuwa nje ...

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages