Kutiwa
saini mkataba huo na Rais Nkurunziza kunamaanisha kujiondoa taifa la
Burundi katika mkataba wa Roma ambao ndio uliunda mahakama hiyo ya
jinai. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, awali tarehe 12 ya mwezi huu bunge la
Burundi lilipasisha muswada wa kujiondoa nchi hiyo kutoka mahakama ya
ICC.
Itakumbukwa
kuwa Burundi ilitia saini mkataba wa Roma mwezi Januari mwaka 1999 huku
ikiupashisha mnamo mwaka 2004. Aidha hatua hiyo ya Rais Nkurunziza hapo
jana, inaifanya Burundi kuwa nchi ya kwanza kujiondoa kwenye mahakama
hiyo.
Serikali
ya Bujumbura inaituhumu Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kuwa ya
kisiasa na ambayo ipo kwa ajili ya kuzikandamiza nchi za Kiafrika pekee.
Mbali na
Burundi, nchi kadhaa za Kiafrika zimetishia kujiondoa kwenye mahakama
hiyo kutokana na hatua yake ya kuendelea kuwasakama viongozi wa nchi za
bara hilo, huku ikifumbia macho jinai zinazofanywa na mataifa waitifaki
wa Magharibi.
No comments:
Post a Comment