Siku chache baada ya Burundi kutangaza
maamuzi ya kujitoa kwenye Mahakama ya makosa ya uhalifu ICC, Umoja wa
Ulaya umetangaza kuitenga serikali ya Burundi kwenye masuala ya fedha za
kikosi chake kilichotumwa nchini Somalia kujiunga na kikosi cha Umoja
wa Afrika kusimamia amani nchini humo (AMISOM).
Umoja wa Ulaya, ambaye ni mfadhili mkuu
wa Burundi unachangia 20% ya bajeti ya taifa hilo, umeamua kuchukua
vikwazo dhidi ya serikali ya Burundi, inayotuhumiwa kwa ukiukwaji mkubwa
wa haki za binadamu na kukataa mpaka sasa kuketi kwenye meza ya
mazungumzo na upinzani wake. Serikali ya Burundi imeendelea kutengwa
katika ngazi za kimataifa, na kutuhumiwa uhalifu mbaya dhidi ya
binadamu, Umoja wa Ulaya unataka kuzuia moja ya sehemu kuu zinazoipatia
serikali ya Burundi fedha za kigeni.
Umoja wa Ulaya umechukua uamuzi wa
kutopitisha tena mishahara ya askari wa nchi hiyo wanaosimamia amani
nchini Somalia kwenye akaunti ya serikali. Uamuzi wa EU unakuja wakati
ambao uchumi wa Burundi umeendelea kudorora, hata baadhi ya shughuli
zinazoingiza mapato kwa serikali zimekwama kutokana na hali mbaya ya
kiuchumi
Ni wiki tatu sasa tangu Umoja wa Ulaya
kutuma fedha kwenye akaunti ya Umoja wa Afrika ili kulipa mishahara
askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).
Ripoti kutoka Brussels Ubelgiji zinasema
Umoja wa Ulaya umelipa tu malimbikizo ya kipindi kinachoishia hadi
Machi 16, 2016, tarehe ambayo Umoja wa Ulaya uliiwekea vikwazo serikali
ya Burundi, kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Mkataba wa Cotonou.
Tangu wakati huo, Umoja wa Ulaya
ulisimamisha misaada yake ya moja kwa moja kwa serikal ya Burundi. Ni
Euro milioni 5 tu za mishahara ya askari 5,500 wa Burundi wa kikosi cha
AMISOM zimekua zikipitishwa kwenye hazina ya serikali ya Burundi
No comments:
Post a Comment