HABARI>>>>SEHEMU YA HOTUBA YA WAZIRI MKUU - G EMPIRE
  • Home
  • About
  • Contact
  • 404

G  EMPIRE

PATA HABARI ,MATUKIOMBALIMBALI KWA WAKATI MUAFAKA KUPITIA HAPA GAMBATHEBOSS

Latest in Tech

test banner
  • Home
    • Seo Services
    • DropDown
    • _DropDown 1
    • _DropDown 2
    • _DropDown 3
    • __DropDown 3.1
    • __DropDown 3.2
    • __DropDown 3.3
    • __DropDown 3.4
    • _DropDown 4
    • _DropDown 5
    • Post Formats
    • _Typography
    • _SiteMap
    • _Full Post
    • _Left Sidebar
    • _Right Sidebar
    • Documentation
    • Download

    Post Top Ad

    Responsive Ads Here
    Home HABARI HABARI>>>>SEHEMU YA HOTUBA YA WAZIRI MKUU

    HABARI>>>>SEHEMU YA HOTUBA YA WAZIRI MKUU

    gambatheboss November 14, 2016 HABARI,
    Share This

    SEHEMU YA HOTUBA YA WAZIRI MKUU BUNGENI WAKATI AKIHAIRISHISHA BUNGE, SIKU YA IJUMAA TAREHE 11/11/2016.
    10. Mheshimiwa Spika, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 10 Septemba, 2016 lilitokea tetemeko la ardhi katika eneo la Kanda ya Ziwa na hususan Mkoa wa Kagera. Tetemeko hilo lilisababisha athari mbalimbali zikiwemo vifo, majeruhi, uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi. Jumla ya Watu 117,721 wameathirika kwa kupoteza makazi yao, mali na athari za kisaikolojia katika Wilaya za Bukoba, Missenyi, Muleba, Karagwe na Kyerwa. Aidha, jumla ya watu 17 walipoteza maisha na 560 walijeruhiwa. Vilevile, nyumba 2,072 za makazi zilianguka kabisa na nyumba 14,595 za makazi zilibomoka, baadhi zina kuta au kupata nyufa kubwa na hivyo kuzifanya kuwa hatarishi kwa makazi ya binadamu. Vilevile, maafa haya yalisababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara na majengo ya Serikali 1,718 yaliyoharibika kwa viwango tofauti.
    11. Mheshimiwa Spika, kufuatia hali hiyo, Serikali ilianzisha Kituo cha Operesheni na Kuratibu Maafa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa lengo la kuharakisha huduma. Aidha, Serikali ilitoa matibabu bure kwa majeruhi wote, kuandaa na kugharamia mazishi ya watu 17 waliofariki ambapo mimi binafsi nilihudhuria na pia kutoa mkono wa pole wa Shilingi Milioni 17 kwa wafiwa. Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali iliwahudumia wananchi walioathirika na tetemeko kwa kuwapatia misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, madawa, nguo, makazi ya muda, vifaa vya ujenzi, vifaa tiba, vifaa vya shule na huduma ya ushauri wa kisaikolojia. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na wadau mbalimbali walifanya Tathmini ya pamoja ya mahitaji ya haraka katika kukabiliana na Athari za Tetemeko hilo. Ambapo utekelezaji wa masuala muhimu yaliyoainishwa katika tathmini hiyo unaendelea.
    12. Mheshimiwa Spika, ili kuwezesha wadau, taasisi na wananchi mbalimbali kuchangia maafa hayo, *Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Kagera ilifungua Akaunti pekee Namba 0152225617300 katika Benki ya CRDB Bukoba yenye jina la “KAMATI MAAFA KAGERA”.* Hadi kufikia tarehe 10 Novemba, 2016 kiasi cha *Shilingi 5,427,671,677.32 kilikuwa kimeingizwa kwenye Akaunti hiyo.* Hadi kufikia tarehe 10 Novemba 2016 Salio katika Benki ni Shilingi 4,296,038,711.79 na matumizi hadi tarehe tajwa yalikuwa ni Shilingi 1,130,428,347.53. Aidha, Kamati pia ilisajili namba za simu za mkononi za kupokea michango katika Kampuni za Vodacom (M-Pesa) 0768 196 669, Tigo (Tigopesa) 0718 069 616 na Airtel (Airtel Money) 0682 950 009 kwa jina la “KAMATI MAAFA KAGERA”. Hadi kufikia tarehe 10 Novemba, 2016, kiasi cha *Shilingi 16,638,747 kilichangwa kupitia mitandao hiyo ya simu.* Hivyo kufanya *jumla ya fedha zilizopokelewa kupitia Benki na Mitandao ya Simu kuwa Shilingi 5,444,310,424.32.* Aidha, Serikali imechangia Shilingi Billioni Moja katika kukabili janga hilo.
    13. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kupokea misaada kutoka kwa Washirika wetu wa Maendeleo, Balozi na hata Nchi marafiki. Mathalan, tumepokea kutoka Serikali ya Uganda Dola za Kimarekani 200,000 sawa na Shilingi Milioni 419.2, Serikali ya India Shilingi Milioni 547, Serikali ya Kuwait Shilingi Milioni 51 na Serikali ya Uingereza iliahidi kutoa Shilingi Bilioni Sita zitakazoelekezwa kwenye ujenzi wa shule.
    14. Mheshimiwa Spika, tumepokea vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 357 yakiwemo maturubai, magodoro, ndoo, mashuka, vifaa tiba, dawa na chakula kutoka Serikali za Japan, China, Kenya, Pakistan, Burundi na Rwanda.
    15. Mheshimiwa Spika, taarifa ya Kikosi Kazi cha Wataalam imeainisha kuwa takribani Shilingi Bilioni 63.2 zitahitajika kurejesha hali ya kawaida katika Mkoa wa Kagera kufuatia maafa hayo. Gharama hii inajumuisha ukarabati wa shule za msingi, sekondari, vituo vya afya na taasisi nyingine katika wilaya zote sita za Mkoa huo, ujenzi mpya wa shule za Ihungo na Nyakato (tayari wafadhili wamejitolea kujenga shule hizi). Aidha, hadi kufikia tarehe 10 Novemba, 2016 kiasi cha Shilingi 966,898,826 zilitumika katika kufanya ukarabati mkubwa na mdogo wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Zahanati katika Halmashauri za Mkoa wa Kagera. Serikali inaendelea na ujenzi wa Zahanati mpya (Ishozi) inayojumuisha chumba cha Upasuaji na wodi ya kinamama na watoto na usimamizi wa ujenzi wa shule za Ihungo na Nyakato. Aidha, katika kuongeza nguvu ya urejeshaji hali jumla ya Askari 96 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwemo Wahandisi, Mafundi, Wapishi, na Madereva waliwasili Mkoani Kagera tarehe 19 Oktoba, 2016 kushiriki katika zoezi la kurejesha hali ya majengo na miundombinu.
    16. Mheshimiwa Spika, Serikali inapenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu na wananchi kwa jumla kuwa Serikali ipo pamoja na waathirika hawa katika suala hili na ina mikakati madhubuti ya kuhakikisha tunarejesha hali bora kwa kuendelea kurudisha miundombinu, kutoa huduma za kibinadamu na matibabu kwa waathirika. Aidha, napenda kuwashukuru wale wote waliochangia katika kusaidia wenzetu wa Kagera, kwani katika kipindi hiki, tumeonesha umoja wetu, upendo wa dhati, hali ya kuthaminiana na kujaliana. Mungu awabariki sana na kuwaongezea pale walipotoa. Kipekee, niwashukuru Nchi marafiki, Balozi, Wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya Nchi, Taasisi za Kiserikali na zisizo za Kiserikali, Taasisi za Fedha, Kampuni, Vikundi mbalimbali, pamoja na Wananchi wote wakiwemo wale waishio nje ya Nchi.


    Tags # HABARI
    Share This
    Author Image

    About gambatheboss

    HABARI
    By gambatheboss at November 14, 2016
    Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
    Labels: HABARI

    No comments:

    Post a Comment

    Newer Post Older Post Home
    Subscribe to: Post Comments (Atom)

    BREAKINK NEWS>>>>.GAMBATHEBOSS IMERUDI HEWANI

         " Tuna ombaradhi wapenzi wa somaji wetu kwa kupotea hewani takribani mwaka mmoja na nusu hivi  kutokana na tatizo lililo kuwa nje ...

    Post Bottom Ad

    Responsive Ads Here

    Author Details

    Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.

    Main Menu

    Socialize

    • facebook count=3.5k;
      Followers
    • twitter count=1.7k;
      Followers
    • gplus count=735;
      Followers
    • youtube count=2.8k;
      Followers
    • pinterest count=524;
      Followers
    • instagram count=849;
      Followers

    Facebook

    G  EMPIRE

    PATA HABARI ,MATUKIOMBALIMBALI KWA WAKATI MUAFAKA KUPITIA HAPA GAMBATHEBOSS

    G EMPIRE

    PATA HABARI ,MATUKIOMBALIMBALI KWA WAKATI MUAFAKA KUPITIA HAPA GAMBATHEBOSS

    Powered by Blogger.

    viwes

    Report Abuse

    Total Pageviews

    Search This Blog

    Find Us On FacebooK

    https://www.facebook.com/mkama.gamba.1
    Most Watch Video

    About us

    Test Footer 2

    Video Of Day

    Flickr Images

    wanao tutembelea

    wanao tutembelea

    ADROID APLICATION

    Downlod my app here kwa habari mbalimbali kama vile michezo
    na Burudani habariza kitaifa na kimataifa ,matukio mbalimbali nk.

    About Me

    gambatheboss
    View my complete profile

    Subscribe Tohttp://gambatheboss.blogspot.com

    Posts
    Atom
    Posts
    Comments
    Atom
    Comments
    Responsive Ads Here

    Most Popular

    • SPORT>>>>YANGA YASAJILI WAWILI
      Timu ya Yanga mesajili wachezaji wawili  ikiwa ni moja ya kukiongezea nguvu kikosi hicho cha wana jangwani Hawa ndio wachezaji walio saj...
    • SPORT >>>>MWENYE YANGA YAKE KARUDI
      ...
    • MPYA >>>>TAZAMA MATOKEO YA DARASA LA SABA
      NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA October 27 2016  Baraza la mitihani la Taifa ...
    • SPORT>>>UKWELI KUHUSU LWANDAMINA
      DONDOO MHIMU KUHUSU GEORGE LWANDAMINA. - Jina lake kamili George Lwandamina. - Tarehe ya kuzaliwa 5 August 1963 ( miaka 53 ) - Alikuwa ...
    • NEW VIDEO FROM LINAH -RAHA JIPE MWENYEWE
      Ihapa kupakua wimbo toka kwa linah sanga raha jipe mwenyewe
    • MPYAAA >>>>> TRUMP ALIVYO ITAMKA TANZANIA
      ...
    • MPYAA >>>> CHADEMA SASA KUTOA MIKOPO ELIMU YA JUU
      Hiyo apo juu ni taarifa ya  CHASO kwa wale wanafunzi walio kosa mikopo kufadhiliwa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA). Kwa ...
    • SPORT >>>>>>>Nahotha wayanga canavaro anena haya
      N Nahadha  wa yanga  sc nadir haroub kanavalo ameamua kuvunja ukimya  na kuwasihi wanachama na wapenzi watimu ya YANGA waondoe wasiwasi...
    • MAGUFULI AMJIBU ZITTO KABWE KUHUSU KUDANGANYA WATUMISHI HEWA
    • SPORT >>>KIKOSI CHA YANGA LEO DHIDI YA MBAO
      YANGA SC V/S MBAO FC UWANJA.UHURU MUDA.SAA 10:00 JIONI KIKOSI CHA YANGA SC 1.DEO MUNISHI DIDA 2.HASSAN KESSY 3.HAJJ MWINYI 4.AND...

    Popular

    • MPYAAA >>>>> TRUMP ALIVYO ITAMKA TANZANIA
      MPYAAA >>>>> TRUMP ALIVYO ITAMKA TANZANIA
      ...
    • HABARI >>>KUTOKA IKULU  RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE
      HABARI >>>KUTOKA IKULU RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE
      Leo  18 Novemba, 2016 amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kager...
    • BREAKINK NEWS>>>>.GAMBATHEBOSS IMERUDI HEWANI
           " Tuna ombaradhi wapenzi wa somaji wetu kwa kupotea hewani takribani mwaka mmoja na nusu hivi  kutokana na tatizo lililo kuwa nje ...
    • SPORT>>>>YANGA YASAJILI WAWILI
      SPORT>>>>YANGA YASAJILI WAWILI
      Timu ya Yanga mesajili wachezaji wawili  ikiwa ni moja ya kukiongezea nguvu kikosi hicho cha wana jangwani Hawa ndio wachezaji walio saj...
    • MAGAZETINI LEO>>>>>SOMA HABARI MBALIMBALI ZA MAGAZETINI
      MAGAZETINI LEO>>>>>SOMA HABARI MBALIMBALI ZA MAGAZETINI
      Leo  December 5 2016 kukusogezea post zote kubwa kwenye magazetini leo pata kusoma habari mbalimbali zikiwemo za kitaifa kimataifa udaku mic...

    Recent

    Comments

    Archive

    Sponsor

    AD BANNER

    Technology

    Tags

    breaking news HABARI habari tanzania happy barthday magazeti MAGAZETINI LEO Michezo music NEWS nwes sport

    Tags

    Connect With us

    Over 600,000+ Readers Get fresh content from FastBlog

    Recent News

    Contact Form

    Name

    Email *

    Message *

    Categories

    Tags

    Pages

    • Home
    Crafted with by TemplatesYard | Distributed by Blogger Themes