HABARI>>>MWILI WA SITTA KUWASILI NCHINI ALHAMIS - G EMPIRE

G  EMPIRE

PATA HABARI ,MATUKIOMBALIMBALI KWA WAKATI MUAFAKA KUPITIA HAPA GAMBATHEBOSS

Latest in Tech

test banner

Post Top Ad

Responsive Ads Here

HABARI>>>MWILI WA SITTA KUWASILI NCHINI ALHAMIS

Share This

Mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel Sitta unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamisi wiki hii kutoka nchini Ujerumani.

 

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu jijini Dar Es Salaam Msemaji wa familia Gerald Mongella amesema mara baada ya mwili huo kuwasili nchini utapelekwa nyumbani kwa marehemu na siku ya Ijumaa shughuli za kuuaga zitafanyika katika viwanja vya KARIMJEE na kisha utapelekwa bungeni mjini Dodoma.

 

Spika mstaafu Sitta alifariki dunia jana alfajiri katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.

Marehemu Sitta anatarajiwa kuzikwa wilayani Urambo mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment

BREAKINK NEWS>>>>.GAMBATHEBOSS IMERUDI HEWANI

     " Tuna ombaradhi wapenzi wa somaji wetu kwa kupotea hewani takribani mwaka mmoja na nusu hivi  kutokana na tatizo lililo kuwa nje ...

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages