Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli leo ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kupata nafuu.
Mama Janet Magufuli kabla ya kuondoka katika Wodi ya Sewahaji alipokuwa amelazwa aliwashukuru Madaktari, Wauguzi na Wafanyakazi wote kwa huduma nzuri walizompatia.
Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara‘

No comments:
Post a Comment