Siku 14 baada ya
Dar es Salaam Young Africans kupitia kwa kaimu katibu mkuu wake
Baraka Deusdedit atangaze kukanusha klabu hiyo kuwa na mpango wa kumfuta kazi
Hans van Pluijm na kurithiwa na kocha wa
Zesco United ya
Zambia George Lwandamina, hatimae leo October 24 ukweli wa taarifa hizo umeanza kufahamika.
Yanga walikanusha kuwa katika mpango wa kumfuta kazi kocha Hans van Pluijm October 10 2016 lakini sasa kuwasili kwa kocha mzambia mchana wa October 23 George Lwandamina Dar es Salaam kunaanza maliza uvumi wa tetesi hizo, Lwandamina tayari yupo Dar es Salaam licha ya kuwa Yanga hawajathibitisha lolote.
No comments:
Post a Comment